Wizkid awapa neno mashabiki zake.

Baada ya kunyakuwa tuzo kadhaa alizowekwa mwaka huu msanii kutoka Nigeria alifanya ngoma nyingi zaidi nchini humo,Wizkid awaomba radhi mashabiki zake aliowaahidi kumaliza nao mwaka kwa show.

Wizkid amepiga show nyingi zaidi kuliko msanii yoyote yule kutoka Nigeria akifuatiwa na Techo. kupitia ukurasa wake wa Instagram. wizkid anatuchana sababu za yeye kupumzika na kutofanya show mwaka huu.

wlm inakusogezea kilichomfanya wizkid kusitisha show zake mwishoni mwa mwaka huu.

 

Itazame hapa mtu alivyotunzwa pesa mbele ya mashemeji zake.
Advertisements

Darassa Ajiwekea Rekodi Mpya Kwenye Muziki Wake.

Uamuzi wa kubadilisha muziki wake, umeendelea kumzalia matunda matamu rapper Darassa. Akiwa na wimbo ambao hakuna anayeweza kubisha kuwa ndio namba moja nchini kwa sasa, Muziki, mkali huyo kajiandikia rekodi yake nyingine katika CV yake.

Video ya wimbo wake huo imefikisha zaidi ya views milioni 1 ndani ya wiki mbili tangu iwekwe kwenye mtandao wa Youtube. Ni nadra sana kwa msanii anayerap kufikisha idadi hiyo ya views katika kipindi hicho.

Wimbo huo kwa muda mfupi umemfanya Darassa awe miongoni mwa wasanii wanaotafutwa sana kwa show wakati huu.

Nay wa Mitego: Mimi na Mr. T Touch Tulishamalizana.

Nay wa Mitego anaweza akawa anamiss midundo ya producer wake wa zamani, Mr T Touch lakini hana mpango wa kufanya naye tena kazi.

Tangu waache kufanya kazi pamoja, rapper huyo amekuwa kimya kiasi na huenda akawa bado hajapata producer mwingine wa kuziba pengo lake. Akizungumza na mtangazaji wa Jembe FM, JJ, Nay amesema kuwa biashara yake na T Touch ilishakwisha.

“Katika suala ambazo huwa sipendi kuzungumzia ni suala la mimi na Mr T, tulishamalizana kama itakuja kutokea basi itakuja kutokea na kila kitu mtu ataona, nadhani hii biashara ya mimi na T ilishaisha,” alisema rapper huyo.

Huu Ndio Muonekano wa Zari The Bosslady Baada ya Kujifungua, Utapenda Hii.

Zari The Bosslady amerudi barabarani siku chache tu baada ya kujifungua mtoto wake wa pili na Diamond.

Akiwa kwenye makazi mapya – kwenye nyumba yao na mchumba wake supastaa iliyopoto Pretoria, SA, mama huyo mwenye watoto watano kwa ujumla, hakutaka kuchelewa kurejea kwenye maisha yake ya kupendeza.

Amepost picha tatu Instagram ambapo ya kwanza akiwa kwenye gari ameandika: When mummy got some errands to run.”

Nyingine anayoonekana akiwa amempakata mtoto huyo wa kiume anayedaiwa kupewa jina ‘Riaz’ (kinyume cha jina Zari), ameandika: Simply do what suits your lifestyle and health in general.”

Nyingine ameonekana akiwa amesimama kwenye mlango wa nyumba yao iliyonunuliwa kwa takriban shilingi milioni 400.